Ijumaa, 8 Juni 2018

ADEN RANGE MARWA WA KENYA ATOLEWA KOMBE LA DUNIA

Refarii wa Kenya Aden Range Marwa ameondolewa kuchezesha mechi za Kombe la Dunia nchini Urusi kwa madai ya rushwa. Marwa ni miongoni mwa watuhumiwa wengine wapatao 100 walionaswa katika mkanda wa video na mwandishi wa Ghana Anas Aremeyaw Anas wakipokea rushwa.

huyu refalii wa kenya Aden

KUTOKA BURUNDI

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amesema hatogombea tena katika uchaguzi wa 2020 na ameahidi kumuunga mkono atakayeteuliwa kugombea urais. Kauli hiyo ameitoa leo wakati akisaini marekebisho ya katiba yanayoweza kumruhusu kubakia madarakani hadi 2034.

Jumatatu, 12 Machi 2018

PIERRE NKURUNZIZA APEWA CHEO NA CHAMA TAWALA

Chama tawala nchini Burundi kimempa cheo cha ''mlinzi aliyetukuka'' rais Pierre Nkurunziza wakati ambapo wakosoaji wake wanadai kwamba anataka kubakia madarakani milele. Katibu Mkuu wa chama tawala cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye amesema kupitia njia ya vidio katika mkanda uliotumwa kwa shirika la habari la AFP na kuthibitishwa na afisa mmoja, kwamba rais Nkurunziza ni mzee wao,baba yao na mshauri wao. Wakosoaji wamelalamikia kilichotokea wakisema kwamba ni kumpa umaarufu wa kuonekana kuwa ni Mfalme Nkurunziza. Kwa sasa kura ya maoni kuhusu Katiba iliyopangwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu huenda ikampa nafasi ya kugombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2020 na kumfungulia njia ya kubakia madarakani hadi mwaka 2034.

Jumatano, 7 Machi 2018

TAARIFA KUTOKA TFDA

Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imesema Tanzania itajiunga na mataifa mengine kuzuia uingizaji wa Soseji kutoka Afrika Kusini zilizobainika kuwa na bakteria aina ya Listeria, iliyosababisha vifo vya watu takriban 180 nchini Afrika Kusini tangu 2017. Tayari Kenya, Zambia, Malawi, Botswana, Zimbabwe, Swaziland na Msumbiji zimepiga marufuku bidhaa za nyama ya kusindika kuingia nchini mwao. Bakteria ya Listeria inasemekana kusababisha homa kali, kuharisha na pia kuwa na athari katika mfumo wa damu.

Jumanne, 27 Februari 2018

CONGO DRC

HABARI Mahakama ya kijeshi kaskazini magharibi mwa DRC imemuhukumu kifungo cha maisha jela afisa wa polisi aliyefyatua risasi na kumuua mmoja wa wandamanaji wanaompinga rais Joseph Kabila. Mjini Kinshasa pia afisa mwingine wa polisi amekamatwa kwa makosa kama hayo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani. Hata hivyo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yamezungumzia kutoridhishwa na kesi hiyo kwa sababu haiwahusishi viongozi wa ngazi ya juu ambao wanaongoza jeshi na polisi.

SAUDI ARABIA

Mfalme Salman wa Saudi Arabia amefanya mabadiliko ya nyadhifa za jeshi na wizara mbalimbali, pamoja na kuteua naibu waziri wa kike akiwa na lengo la kuingiza kizazi kipya serikalini. Ufalme wa Saudia haukutoa sababu za kutokea mabadiliko hayo na wala haukutoa maelezo yoyote juu ya namna inavyopanga kuimarisha Wizara yake ya Ulinzi. Katika wakati ambapo Ufalme wake unakosolewa kimataifa kwa kuongoza mashambulizi ya anga nchini Yemen yanayoua raia wa kawaida kwa kulenga masoko, hospitali na maeneo mengine ya raia. Watu wapatao 10,000 wameuawa katika vita hivyo ambavyo Saudi Arabia inaiunga mkono serikali inayotambuliwa kimataifa dhidi ya waasi wa Houthi wanaoudhibiti mji mkuu wa Sanaa kwa sasa. Makundi ya kutoa misaada ya kiutu yanailaumu Saudia kwa kuitumbukiza Yemen katika baa la njaa.    www.wbca.st/R9iKxw

Ijumaa, 16 Februari 2018